Fikra Pevu Darasa
Darasa La Fikra Pevu 2017
Kitabu hiki ni zao la darasa la fikra pevu ambalo lilifanyika mwaka 2017 likiwa na jumla ya watu 103 na kuendeshwa kwa siku zipatazo 30 kwa kuwa na masomo ya asubuhi saa kumi na mbili kwa kuwa muundo wa tafakari na wakati wa jioni kuwa ni muda wa tafakari katika yale ambayo katika siku mtu huyo amejifunza na kutendea kazi. Pia jioni ulikuwa ni wakati mzuri sana wa tafakari katika picha na kushirikishana masomo husika. Hivyo unapokuwa wasoma kitabu hiki ambacho ni kusanyo za masomo ambayo ukiweka nguvu na uzito katika kuyatenda basi kuna hatua kubwa sana ambayo utaivuka na kufanikiwa katika mipango yako. Katika kusoma hiki kitabu utakutana na tafakari za asubuhi, tafakari za jioni na pia masomo na chambuzi za vitabu. Unaweza kusoma k wa namna upendavyo na kuchukua hatua ni kazi yako ili upate matokeo makubwa ambayo umekuwa unatamani kupata.