FANIKIWA
MAMBO 150 YATAKAYOKUINGIZA KWENYE AINA YA MAFANIKIO UNAYOYATAKA
Kila mtu anatamani kufanikiwa au kufikia malengo aliyonayo. Ufafanuzi wa mafanikio umetofautiana kutoka mtu mmoja hadi mwingine kulingana na jinsi kila mtu alivyo. Tukiachilia mbali maana halisi ya mafanikio pamoja na nguzo zake muhimu, mafanikio ni mchakato ambao hujumuisha mambo mengi sana.
Kwa kifupi mafanikio ni mfano wa chakula kitamu (kizuri) ambacho ndani yake kuna mkusanyiko wa virutubisho vya aina nyingi ambapo kila kimoja kina kazi yake maalumu. Pia ni mfano wa mtumbwi ambao kusogea kwake mbele hutegemea uwiano wa upigaji wa makasia pande zote kwa idadi fulani na hauwezi kusogea ikiwa kasia litapigwa kwa upande mmoja tu. Hivyo ikiwa kirutubisho kimoja tu hakimfanyi mtu kuwa na afya bora na kupiga kasia upande mmoja kwa bidii hakuwezeshi mtumbwi kusonga mbele kwa uelekeo sahihi vivyo hivyo mafanikio hayaletwi kwa kushikilia kitu kimoja tu. Ila kwa uwiano mzuri wa mambo yaletayo mafanikio mtu anaweza kufanikiwa
Wahenga walisema, “chembe na chembe mkate huwa”, “haba na haba hujaza kibaba” na semi nyingine nyingi zinazofanana na hizi wakiwa na maana kuwa kitu kikubwa kinaweza kutengenezwa pale vitu vidogo vinapokusanyika pamoja. Kitabu hiki kinagusia baadhi ya mambo muhimu ambayo ukiyaleta pamoja katika uwiano mzuri na stahiki yanaweza kukuingiza katika aina ya mafanikio unayoyataka na kukufanya uishi kwa amani na furaha.
Ukiweza kusoma kitabu hiki na kuyafanyia kazi yaliyomo, mafanikio yatakuwa na sehemu ya maisha yako.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza