Diwani Ya Nchi Ya Mbali
Diwani Ya Nchi Ya Mbali
Diwani Ya Nchi Ya Mbali ni mkusanyiko wa mashairi ya aina mbalimbali yenye kuangazia masuala muhimu katika nchi ya mbali. Mkusanyiko wa mashairi haya unakuwa wenye umuhimu mkubwa sana na unaifanya diwani hii kuwa yenye msaada kwa walimu wa wanafunzi wa fasihi kwenye kufundisha na kujifunza Ushairi kwa ngazi mbalimbali ikiwamo chuo kikuu. Diwani hii hailitengi kundi la aina yoyote, kwani hata mtu asiye mwanafasihi akiisoma diwani hii ni yenye tija na kumfanya awe huru kifikra. Diwani hii ni yenye kumfanya mtu akapata nuru kwenye fikra zake na kuweza kuwaza nje ya kasha. Msukumo wa kutunga mashairi ulitokana na tajiriba ya Mwandishi kwa kupenda ushairi, kuwa na kipawa cha kutunga mashairi na pia kuwa mwanafunzi mzuri katika uga wa fasihi na zaidi sana diwani hii ni zawadi ya mtunzi katika kuikuza na kuiendeleza fasihi. DIWANI YA NCHI YA MBALI ni tunu katika Fasihi Simuilizi na Andishi ya Kiswahili. Diwani hii imesheheni mashairi ya aina mbalimbali na yenye mifano ya vipengele mbalimbali vya fani kwa kufundishia na kuijfunza ushairi. Pia maudhui yaliyomo kwenye diwani hii ni faafu kuionya na kuiadibisha jamii na kuufanya ulimwengu kuwa paradiso ndogo.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza