Dira Ya Taifa: Barabara Ambayo Hatujawahi Kuisafiria
Kitabu hiki kinahusu utawala bora nchini Tanzania. Kimeandikwa kwa ajili ya kujaza au kuondoa kabisa bonde lilipo kati ya mifumo ya kisiasa, kiutawala na kiuchumi nchini mwetu.\\\\r\\\\n\\\\r\\\\nBonde hili limesababisha kuwepo kwa dhana mbalimbali za utawala bora. Kwa kuwa maendeleo ni zao la utawala bora wa mahali husika basi kuna haja ya kuwa na dhana moja shirikishi kuhusu utawala bora ili kurahisisha ushirika wa watu wote katika maendeleo.\\\\r\\\\n\\\\r\\\\nAidha kitabu hiki kimekusudiwa kuingiza ufahamu, ujuzi na mtizamo mpya kwa waandaa sera na wananchi kwa ujumla kuelekea dhana moja ya kitaifa katika misingi ya utawala bora.Kusudi hili litazamiwe kama ufunguo muhimu kabisa katika kujenga uwezo mpya kwa ajili ya mabadiliko mapya ya kitabia, mitizamo na sura ya nje katika mambo yote yahusuyo utawala bora kwa maendeleo ya Taifa.\\\\r\\\\n\\\\r\\\\nKitabu kimeandaliwa katika namna ambayo inaashiria au kuelekeza uhusuano wa ujumla kati ya mifumo hiyo tajwa hapo juu na uwezeno wa kuiakisi katika mchakato wa kuliendeleza taifa letu kiuongozi.Ikiwa msomaji wangu atamaliza sura zote na akaelewa kinaga ubaga kabisa juu ya dhana hii mpya ya utawala bora basi dhumuni la kitabu hiki litakuwa limefikiwa.\\\\r\\\\n\\\\r\\\\nNakutakia safari njema kuelekea utawala bora nchini mwetu.
Siasa, uongozi , uchumi, maendeleo na utawala Bora!
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza