DIRA YA KUJIAJIRI
DIRA YA KUJIAJIRI
Ni kitabu kilichoandikwa kwa lengo la kutoa mwongozo mwepesi utakaomwezesha kila mwenye nia ya kujiajiri akiwemo mjasiriamali, mhitimu au hata mwajiriwa ili ajiajiri katika shughuli yoyote anayoipenda ili aweze kujiingizia kipato na kujiimarisha Kiuchumi.
WAHITIMU wengi wanashindwa kujiajiri kwa kukosa mwongozo mzuri utakaowawezesha kujiajiri na wanabaki hawana ajira kwa kuwa miaka ya hivi karibuni kumekuwa na changamoto ya ajira rasmi serikalini na hata mashirika binafsi kutokana na kuwa na wasomi wengi wa ngazi mbalimbali za elimu.
Kupitia kitabu hiki WAJASIRIAMALI watapata maarifa na mwongozo ili waweze kujiajiri katika Miradi au Maeneo mbalimbali wanayoyapenda na kujiingizia kipato hatimaye kujiimarisha kiuchumi.
WAAJIRIWA wakisoma kitabu hiki watapata mwongozo wa namna kujiajiri katika kazi ya ziada wanazozipenda ili waweze kujiingizia kipato na waweze kukidhi mahitaji yao na hata kufikia kuweka akiba.Waajiriwa wengi wamekuwa wakiishi kwa kutegemea mshahara ambao mara nyingi hakuna akiba baada ya matumizi ya mshahara, hivyo wamekuwa wakiishi maisha ya kujirudia rudia na wakijipa matumaini kwa kusema \"nakula, naishi na kulala\" basi inatosha, jambo ambalo linawafanya wasipige hatua ya kimaendeleo miaka mingi, wengine huishi kwa mikopo.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza