DENI LA DHAHABU
Hujazaliwa kulipa bili na kuondoka, dunia inahitaji alama yako.
Mafanikio hayachagui watu. Watu ndio wanachagua kufanikiwa au kutokufanikiwa. Mafanikio yana kanuni zake ambazo yeyote akizifuata, haijalishi ni dini gani, jinsia gani wala elimu gani mafanikio yanampokea. Kama una matatizo au changamoto katika maisha yako, tambua kwamba kuna kitu hakiko sawa na ili changamoto hiyo iondoke lazima ufanye kitu ambacho kitabadilisha changamoto hizo kuwa fursa. Wakati watu waliofanikiwa wanatumia mikopo kufanikiwa zaidi, mikopo hiyo ni changamoto kubwa inayowasumbua watu wa hali ya chini kuliko hata magonjwa.
huwezi kuwa na lengo la kufanikiwa kiuchumi kama bado umekumbatia madeni mabaya. ili ufanikiwe lazima ulipe madeni haya wakati unawekeza kwa ajili ya mafanikio tarajiwa. kitabu hiki kitakupa mwongozo wa jinsi ya kulipa madeni yako yote bila kujali ni kiasi gani na kuwekeza katika miradi na mali zitakazokuingizia kipato kuelekea mafanikio yako ya kiuchumi.
\\r\\n\\r\\nWatu wengi wameishi kwenye utumwa muda mrefu, wanatamani kujitoa katika hali hiyo lakini wanashindwa kulipa gharama ya uhuru wanao utamani. Mafanikio hayana majadiliano, yanakutaka uchague kufuata\\r\\nkanuni na ufanikiwe au uendelee na visingizio vya siku zote na ubaki unalipa bili mpaka uzeeni. kitabu hiki ni usafiri kuelekea katika uhuru wa kiuchumi.