Your Basket

Checkout | Shopping Cart
Dealing With Addictions - GetValue
Biashara & Ujasilimia Mali

DEALING WITH ADDICTIONS

0
0
  • 5
  • 4
  • 3
  • 2
  • 1
Price:
10,000 Tsh.
Added To Cart:
0
Added to shop:
Aug 26, 2024
Product Views:
18
In category:
Sample

Yapo mambo na zipo tabia ambazo kiuhalisia watu huwa hawapendi kuzitenda na huwa wanahangaika sana ili kuweza kutoka bila mafanikio yeyote. Japokuwa na kuhangaika kote bado hujikuta wanarudia tena na tena, Neno la Mungu linasema katika; Warumi 7:15 \"Maana sijui nifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda”.Kitabu hiki ulichokishika mkononi mwako cha \\\"DEALING WITH ADDICTIONS\\\" ni kitabu ambacho kimejaa maarifa na hekima za Mungu katika kuwakomboa watu wake wanaoteseka na vifungo vyote vya uraibu.Neno la Mungu linasema katika kitabu cha; Yohana 8:36 \"Basi Mwana akíwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.\\\" Kwahiyo inaweza kuwa umeteseka sana katika kutafuta wanasaikolojia na watu ili akusaidie kutoka katika uraibu ulio nao lakini unaona hakuna mabadiliko yeyote. Wanasaikolo jia watakupa dawa na mambo ya kutenda lakini ni Yesu pekee ndiye anayeweza kuwafungua watu na akiwafungua yeye watu huwa huru siku zote. Kitabu hiki ni kitabu ambacho kitakupa muongozo wa kiroho kulingana na Neno la Mungu namna ambavyo wewe utatoka katika kila aina ya uraibu unaokusumbua. Pamoja na hilo ni kitabu kilichojaa maombi ya kutosha ambayo utayatumia kuomba na kujiombea wewe mwenyewe mpaka pale utakapoona vile vifungo vinakuachia kabisa. Biblia inatukumbusha katika kitabu cha; Yeremia 32:27 \"Tazama, mimi ni BWANA, Mungu wa wote wenye mwili; je! kuna neno gumu lolote nisiloliweza?\\\" Kwahiyo mwanangu, haijalishi umeteseka miaka mingapi ndani ya uraibu, inawezekana hata wanadamu wameshakukatia tamaa lakini hakuna linalomshinda Mungu. Ninawaombea sana kwa Mungu kuwa kila atakayesoma na kuomba maombi yaliyomo katika kitabu hiki basi Mungu akamuweke huru kabisa. \"Mungu wangu ninayemtumikia hatakuacha uendelee kuteseka tena na uraibu kwa jina la Yesu.\\\" Amen!

Uraibu ni moja ya tatizo kubwa sana ambalo linawatesa sana vijana wengi. Ubaya ni kuwa wachache kati ya hao wanaweza kutafuta msaada wa karibu kutoka kwa wanasaikolojia au wachungaji. Wengi ambao mimi binafsi nimewajua wakiwa matatizo haya sio wepesi wa kutafuta msaada kutoka nje.

Wengi wao hujisikia aibu, hujiona hawafai na wengine wanaona ni kama jambo la kujishushia heshima kusema mambo yao ya ndani kwa watu wengine na hii ndio sababu ambayo inawafanya wengi wanaendelea kuteseka na uraibu. Nina uhakika kwa asilimia kubwa kuwa hata wewe unayesoma hiki kitabu ni mmoja wa watu ambao wamekuwa wakiteseka sana na uraibu na umeteseka bila ya kuweza pata msaada kutoka kwa watu wengine.

Neno la Mungu linasema katika kitabu cha; 

Mathayo 11:28-30

“Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.”

Nimeona watu waliotafuta msaada kwa wanasaikolojia kuhusu uraibu unaowasumbua katika maisha yao lakini baada ya muda walirudi kulekule.

Nimeona watu waliotafuta msaada wa kushinda uraibu kutoka kwa wachungaji na marafiki zao wa karibu lakini matokeo yake walirudi kwenye vifungo vilevile.

Nimewaona watu waliofunga na kuomba lakini bado hawakuweza kushinda uraibu.

Sasa nini kinaweza kukufanya ushinde?

Njia pekee itakayokusaidia wewe kushinda ni kukubali kumtwisha Yesu mizigo yako ya uraibu inayokuelemea na ndipo yeye atakupumzisha na kukuweka huru. Shida kubwa uliyo nayo ni kuwa unafikiri wewe mwenyewe kwa nguvu zako na elimu yako ya darasani itakusaidia kuushinda mwili wako.

Tukumbuke neno la Mungu linasema;

Mathayo 26:41

“Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.”

Wagalatia 5:16-17

“Basi nasema, enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.

Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.”

Mwili sikuzote hutenda kazi na Roho, kwahiyo haijalishi utaomba mara ngapi au utafunga mara ngapi au utakutana na wanasaikolojia wangapi wa kukushauri hii haibadilishi ukweli kuwa huo mwili wako kila mara unashindana na Roho yako.

Niliandika kitabu hiki ili kikawe msaada wa walio wengi ambao wanateseka na uraibu lakini hawaoni namna ya kutoka hapo na pia wanashindwa kutafuta msaada kwa watu wanaowazunguka kutokana na sifa zao na namna ambavyo wanaonekana na watu wengine.

Mwingine anajiwazia mimi ninavyoimba na kuabudu hivi, nitawezaje kumshirikisha mtu kuwa ninahangaika na tatizo la masturbation?

Mwingine akijiangalia yeye ndio kiongozi wa maombi kanisani lakini anateseka na pombe na anakunywa kwa siri bila wengine kujua na kila akitafuta njia ya kuacha hawezi na kuwaambia wengine wamsaidie anaona ni kama fedheha; Inawezekanaje kiongozi wa maombi awe mlevi?

Mwingine ni kiongozi na ana sifa nzuri mbele za watu, anajiwazia atawezaje kusema anahangaika na tatizo la uraibu wa kuangalia picha za utupu?

Nisikilize mwanangu, wewe hautaangamia na wanaoangamia. Maadamu umepata kiu na unatamani kutoka hapo ulipo basi mimi ninakuombea kwa Mungu kuwa utakaposoma na kuomba maombi yaliyomo humu basi uponyaji uingie ndani yako kwa jina la Yesu na ninakuombea uwekwe huru kwelikweli. 

Hivyo kitabu hiki kitaenda kukuongoza hatua kwa hatua na kwa maombi ni kwa namna gani utaweza kutoka katika uraibu lakini pia ni nini ufanye ili usijikute umerudi tena kwenye uraibu na utajifunza juu ya mambo ya kuyaepuka ili usiingie katika uraibu kabisa.

Kwahiyo hakikisha unakisoma kitabu hiki ukiwa na utayari wa kupokea ukombozi wako. Nina uhakika hautateseka tena kama mwanzo na utawekwa huru kwelikweli.

Lakini pia nikusihi na kukuomba wewe mwanangu kuwa balozi mzuri wa Neno la Mungu kwa watu wengine. Kama una rafiki yako au ndugu yako na anateseka na aina yeyote ya tabia ambayo imegeuka na kuwa uraibu hebu mnunulie kitabu hiki kiwe kama zawadi kwake na ufanyike sehemu katika kazi hii ya Mungu. Utakapokuwa sababu ya wengine kuwa huru na kufunguliwa ndivyo ambavyo Mungu anaendelea kukubariki wewe na kukuinua.

Mungu akubariki sana.

More Products On Discount
6,000 Tsh. 5,000 Tsh.

Sold by: Godius Rweyongeza

7,000 Tsh. 2,999 Tsh.

Sold by: Said Maumba

98,000 Tsh. 60,000 Tsh.

Sold by: Prophet Pd John

25,000 Tsh. 10,000 Tsh.

Sold by: Msafiri Lwihula

5,000 Tsh. 2,500 Tsh.

Sold by: Joyce Mwakajonga

More Products From This Seller
Best Sellers List
Best Seller
2,000 Tsh.
(5.4)

Sold by: Gaston Ngailo

Best Seller
10,000 Tsh.
(69.8)

Sold by: Samuel Macha

Best Seller
3,000 Tsh.
(16.4)

Sold by: ABDULKADIR MASSA

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PETER TARIMO

Best Seller
4,000 Tsh.

Sold by: Mashaka Khamis

GetValue Recommendations
Old is Gold