Your Basket

Checkout | Shopping Cart
Christian In Business World - GetValue
Biashara & Ujasilimia Mali

CHRISTIAN IN BUSINESS WORLD

0
0
  • 5
  • 4
  • 3
  • 2
  • 1
Price:
10,000 Tsh.
Added To Cart:
0
Added to shop:
Aug 27, 2024
Product Views:
29
In category:
Sample

Moja ya maswali mengi ninayokutana nayo kutoka kwa wanangu wa kiroho ni kuwa; \"Inawezekanaje watu wa duniani wanaonekana wana mafanikio makubwa katika kazi zao, biashara zao na maisha yao kiujumla kuliko watu ambao wanasema wanamjua Mungu?\" Jambo ambalo watu wengi hawalijui ni kuwa; watu wa duniani wana njia zao ambazo kwao wakizitumia katika maisha yao wanafanikiwa na sisi tuliokoka tunazo njia zetu ambazo tukizitumia tunafanikiwa pia. Neno la Mungu linasema katika kitabu cha;1 Wakorintho 10:3-4 \"Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)\\\" Kwahiyo ijapokuwa tupo duniani njia zetu tunazopaswa kutumia ni tofauti na watu wa duniani. Shida kubwa ya wakristo wengi ni kutaka kufanya biashara zao na mambo yao kama watu wa dunia hii. Kwa namna hiyo kamwe hawawezi kuona matokeo yeyote. Kitabu hiki cha \\\"CHRISTIANS IN THE BUSINESS WORLD\\\" ni kitabu ambacho kimetoa muongozo wa kutosha wa hekima, maarifa na ufahamu wa Kimungu wa namna ya kufanikiwa kibiashara kama mkristo. Kitabu hiki kimeandika pia juu ya siri na kanuni zitakazomuwezesha mkristo yeyote kufanya vizuri katika ulimwengu wa biashara na kufikia mafanikio makubwa.Zaidi ya yote kitabu hiki kimeambatanishwa maombi ambayo wewe kama mfanyabiashara unaweza ukayatumia kuombea biashara yako na bidhaa zako lakini pia Kuna mkusanyiko wa matendo ya kiimani (signs and tokens) ambazo nazo zitakusaidia kupata matokeo mazuri katika biashara zako. Neno la Mungu linasema katika kitabu cha Hagai 2:8 \"Fedha ni mali yangu, na dhahabu ni mali yangu, asema BWANA wa majeshi. Hivyo wewe kama mtoto wa Mungu ni haki yako kufanikiwa katika kila unachofanya. Mimi kama mchungaji wako ninakuombea Mungu akakusaidie na kuendelea kubariki kazi za mikono yako siku zote, Amen.

Kitabu hiki cha “CHRISTIANS IN THE\\r\\nBUSINESS WORLD” ni kitabu kilichojaa hekima na maarifa na mafundisho ya kimungu juu ya eneo zima la biashara na mafanikio kuchumi kupitia biashara.

Jambo nililogundua ni kuwa; watu wengi sana katika karne hii wamejikita katika kujiajiri kupitia biashara na ujasiriamali na kati ya watu hao wakristo ni moja ya watu ambao pia hujihusisha katika biashara. Lengo kubwa la kuandika kitabu hiki ni kuwasaidia wakristo wote na kuwapa muongozo sahihi wa namna ya kupata mafanikio katika biashara zao.

Watu wa huku duniani wao wana njia zao na mbinu zao ambazo huwa zinawasaidia katika kufanikiwa kibiashara. Wapo wanaoua mama zao na watoto wao ili wafanikiwe kibiashara, wapo wanaotoa sadaka kwa miungu mingine ili wafanikishwe kibiashara na wapo ambao wanaenda kwa waganga ili tu wapate mafanikio ya kibiashara. Sasa watu wa duniani wana njia zao na sisi watu wa Rohoni au wakristo tuna njia zetu ambazo kama tukizitumia hizo tutaona na kupata mafanikio makubwa sana katika biashara zetu.

Kabla hatujaenda mbali zaidi kuna maswali baadhi ambayo nilijiuliza kwa undani kabla sijaandika kitabu hiki.

~Ni kwanini wakristo wafanye biashara?

~Kwanini sisi tuwe matajiri?

~Ni kwanini sisi wakristo inatupasa kuwa na nguvu ya kiuchumi?

Ukisoma katika Biblia watumishi wengi wa Mungu walikuwa na nguvu kiuchumi. Wengi Mungu aliwapa kumiliki ng’ombe, mifugo, fedha na mali nyingi sana. Baadhi ya watumishi hawa wa Mungu ni pamoja na Ibrahimu, Yakobo, Suleiman, Yusufu, Ayubu na wengineo.

Kwahiyo kuokoka au kuwa upande wa Mungu sio sababu ya sisi kuishi maisha duni kama wengi wanavyoamini katika jamii zetu kuwa; walokole wengi huwa maskini. Wengi ni maskini na hawana mafanikio kwa sababu hawafuati sheria na kanuni zao kama watu wa dunia hii wanavyofata sheria na kanuni za ufalme wao. Kuwa tajiri na nguvu ya kumiliki ni mpango wa Mungu mwenyewe tangu anamuumba mwanadamu. Tunaona katika kitabu cha;

Mwanzo 1:26-28

“Mungu akasema, na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.”

Kwahiyo sisi tulipewa nguvu ya kumiliki na kutawala vyote vilivyopo nchi kavu na baharini na hivyo ni haki yetu kufanikiwa kibiashara maana nguvu hiyo ya kumiliki na kutawala imo ndani yetu. Lakini ili tuweze kuyaona hayo mafanikio ni lazima tufuate sheria na kanuni zote za kiroho za kutusaidia kufanikiwa ambazo kitabu hiki kimeziandika siri hizo na kanuni hizo kwa undani kabisa. Tunasoma katika kitabu cha;

Hagai 2:4-8

“Lakini sasa uwe hodari, Ee Zerubabeli, asema BWANA; nawe uwe hodari, Ee Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, nanyi iweni hodari, enyi watu wote wa nchi hii, asema BWANA; mkafanye kazi, kwa kuwa mimi ni pamoja nanyi, asema BWANA wa majeshi; kama neno lile nililoagana nanyi mlipotoka katika nchi ya Misri; na roho yangu inakaa kati yenu; msiogope. Kwa maana BWANA wa majeshi asema hivi, Mara moja tena, ni kitambo kidogo tu, nami nitazitikisa hizo mbingu, na hii nchi, na bahari, na nchi kavu; nami nitatikisa mataifa yote, na vitu vinavyotamaniwa na mataifa yote vitakuja; nami nitaijaza nyumba hii utukufu, asema BWANA wa majeshi. Fedha ni mali yangu, na dhahabu ni mali yangu, asema BWANA wa majeshi.”

Tukisoma katika kitabu hiki tutagundua kuwa, Mungu mwenyewe ndiye aliyetoa maagizo kuwa watoto wake wakafanye kazi, wakafungue biashara, wakafungue makampuni na wakajiajiri kwa sababu Mungu atakuwa na wao na atawafanikisha maana fedha na dhahabu ni mali ya Mungu.

Hivyo sababu nyingine inayotufanya sisi wakristo tukafanye kazi na tuingie katika biashara ni kwa sababu ni agizo la Mungu mwenyewe na tuna uhakika wa ahadi ya Mungu kuwa atakuwa pamoja na sisi.

Ukiachana na kuwa ni agizo la Mungu sisi kama wakristo tunaishi duniani na duniani kuna mifumo mingi ambayo inayotuwezesha sisi kuishi vizuri ambayo mifumo hii inahitaji sisi kuwa na fedha. Ijapokuwa duniani sisi tunapita bado tunahitaji kuwa na nguvu ya kiuchumi ili tuweze kuishi vizuri kabla ya unyakuo wa kwenda mbinguni.

Ndani ya kitabu hiki utajifunza juu ya;

  • Kanuni za kiroho ambazo wewe kama mfanyabiashara mkristo zitakusaidia kufanikiwa na kuona matokeo makubwa.
  • Siri za kiroho zitakazokuwezesha kufanikiwa katika eneo la biashara.Pamoja na kujifunza mambo haya ya msingi nimeambatanisha kitabu hiki na muongozo wa maombi ambayo wewe binafsi utayatumia kwa ajili ya kuombea biashara yako kwa undani.

Jambo ambalo huwa nawafundisha sana wanangu wote wa kiroho ni kuwa na uwezo wa kujiombea wenyewe bila kumsubiria mchungaji au nabii. Kwahiyo maombi yaliyomo katika kitabu hiki ni maombi ambayo yatakusaidia sana katika kutafuta na kupata matokeo mazuri katika biashara yako kila siku.

Zaidi ya yote Mungu akubariki sana na akakufanikishe sana katika kazi ya mikono yako na biashara yako kama Neno la Mungu linavyosema katika kitabu cha;

Kumbukumbu la torati 28:3-6

“Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani. Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, maongeo ya ng’ombe wako, na wadogo wa kondoo zako. Litabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga. Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo.”

More Products On Discount
5,000 Tsh. 1,000 Tsh.

Sold by: RAMV MRUMA

98,000 Tsh. 60,000 Tsh.

Sold by: Prophet Pd John

3,999 Tsh. 1,999 Tsh.

Sold by: Daudi Lubeleje

25,000 Tsh. 10,000 Tsh.

Sold by: Msafiri Lwihula

6,000 Tsh. 5,000 Tsh.

Sold by: Godius Rweyongeza

5,000 Tsh. 2,500 Tsh.

Sold by: Joyce Mwakajonga

More Products From This Seller
Best Sellers List
Best Seller
2,000 Tsh.
(5.4)

Sold by: Gaston Ngailo

Best Seller
10,000 Tsh.
(69.8)

Sold by: Samuel Macha

Best Seller
3,000 Tsh.
(16.4)

Sold by: ABDULKADIR MASSA

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PETER TARIMO

Best Seller
4,000 Tsh.

Sold by: Mashaka Khamis

GetValue Recommendations
Old is Gold