Chozi
Natamani ningekuwa kuku naletewa chakula kutwarnnzima na kisha usiku kulala. Natamani ningekuwarnsisimizi ambao wenye ushirikiano na upendo baina yao ilarnninapoona sisimizi wakikanyagwa na kuku wakichinjwarnnakujua kwamba kuwa wao wangependa wawe binadamurnkama mimi. Basi naridhika na Mwenyezi Mungu alivyornniuumba na kama mateso na mitihani ni sehemu yarnmaisha basi nitapambana nayo na kwenye hii vita narnimani nitakuwa mshindi.
Chozi ni riwaya inayomzungumzia Asia, ambaye anapitia mikasa mbalimbali katika maisha na kupambana nayo na kuibuka mshindi dhidi ya maadui zake na hali ngumu ya kimaisha.
Asia anampoteza baba yake na hali kuzidi kuwa ngumu kwa upande wa famiilia yake. Anabahatika kuchaguliwa kuwa mmoja ya wasichana ambao watakoenda mjini kupata elimu. Kufika mjini anakutana na vitu tofauti na kuingizwa kwenye biashara ya ngono. Kwenye biashara ya Ngono anakutana na Jordan ambapo wote wanapata hisia za kimapenzi walipoonana kwa mara ya kwanza. Tabia ya Jordan kuwa mbaya ikambidi Asia atoroke na aanze kutangatanga mjini na ndipo akakutana na Anti Aziza. Kwa Anti Aziza akawa anaishi vizuri na kuona ndoto zake zimetimia hapo. Anapata nafasi ya kufanya kazi kama kijakazi kwenye familia ya kitajiri yenye mshahara mzuri.
Familia hiyo ni familia ya Jordan na Mama Jordan anampenda Asia alivyokuwa na tabia nzuri ila hataki aolewe na Jordani kwani ana rafiki yake ambaye ana mtoto wa kike na ndo huyo anataka aolewe na Jordan.
Karibu usome Chozi ili uweze kuburudika, kusikitika, kutahamaki, kuelimika, kustaajabishwa na la muhimu i kupata funzo katika maisha yako halisi
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza