BARIDI YA MOTO
BARIDI YA MOTO ni kitabu kinachomuelezea binti Venia anayeishi uswahilini katika Maisha ya kiwango cha chini kiuchumi kwa muda mrefu. Hana kazi/ajira ya kuaminika inayoweza kumudu Maisha yake ya kila siku. Anatafuta ajira na baadaye anabahatika kuajiriwa katika kampuni moja ya usafi na hapo ndipo Maisha yake yanabadilika. Fuatilia kitabu hiki ili kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutambua nafasi yako katika mafanikio unayoyapata. Fuatilia simulizi hii kutoka kwa mwandishi Frida Nkarage.
Ni jumamosi ya saa tatu na dakika kadhaa asubuhi ambapo Venia anakurupuka usingizini baada ya kushituliwa na kelele zilizokuwa zinasikika nje huku zikiambatana na honi za pikipiki zilizokuwa zinapigwa mfululizo na bila utaratibu. Venia anafungua pazia la dirisha na kuchungulia nje na haoni sura ya mtu anayemfahamu. Ndipo anakazana kukodoa macho na kutega masikio kwa makini ili kujua nini kinaendelea lakini nanashindwa kuelewa chochote kutokana na kelele zilizojaa na zisizo na mpangilio. Ndipo anaamua kufungua dirisha na kutega masikio kwa umakini zaidi lakini haelewi nini kinaendelea zaidi ya kusikia sauti zinazopishana bila utulivu. “Hapa napitwa sasa, ngoja niende hukohuko nikashuhudie kinachoendelea.\" Venia anajisemea huku akitafuta kandambili uvunguni mwa kitanda ambapo alifanikiwa kuiona kandambili moja tu. “Sasa nyingine itakuwa wapi?.. Ghafla anasikia sauti zinaongezeka.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza