Your Basket

Checkout | Shopping Cart
Amsha Uwezo Wako Halisi - GetValue
Biashara & Ujasilimia Mali

AMSHA UWEZO WAKO HALISI

0
0
  • 5
  • 4
  • 3
  • 2
  • 1
Price:
10,000 Tsh.
Vendor:
Added To Cart:
0
Added to shop:
May 13, 2022
Product Views:
1,164
In category:
Sample

Tambua na Tumia Nguvu Kubwa Iliyolala Ndani Yako Kufanya Makubwa Zaidi

Ukiiangalia punje ya harage unaweza kuona ni\\\\r\\\\nkitu kidogo na cha kawaida kabisa. Ukichukua punje hiyo na kuiweka kwenye meza,\\\\r\\\\nitakaa pale bila ya kuwa na mabadiliko yoyote. Hakuna chochote\\\\r\\\\nkitakachokuonyesha kama ndani ya punje hiyo kuna kitu kikubwa.

Ni mpaka utakapochukua punje hiyo na kuipanda\\\\r\\\\nkwenye ardhi, kuinyeshea maji na kuiwekea mbolea. Hapo itachipua na kutoa mche,\\\\r\\\\nambao ukitunzwa vizuri utatoa punje nyingi za maharage.

Hebu jionee hapo, punje moja ya harage ambayo\\\\r\\\\nunaweza kuiona haina kitu kikubwa, inapokuwa kwenye mazingira sahihi inazalisha\\\\r\\\\npunje nyingi za maharage. Hicho ni kiashiria kwamba ndani ya punje ya harage\\\\r\\\\nkuna uwezo mkubwa ambao umelala tu. Uwezo huo hauwezi kuamka mpaka pale\\\\r\\\\nunapokutana na mazingira sahihi.

Hivyo pia ndivyo sisi binadamu tulivyo,\\\\r\\\\nunaweza kuwa umeshaaminishwa kwamba wewe ni mtu wa kawaida na huna uwezo wa\\\\r\\\\nkufanya chochote kikubwa. Lakini huo siyo ukweli, ndani yako una uwezo mkubwa\\\\r\\\\nsana ambao umelala tu.

Uwezo huo umelala kwa sababu haujapata\\\\r\\\\nmazingira sahihi ya kustawi na kuzalisha matokeo makubwa. Kama tangu ukiwa\\\\r\\\\nmtoto umekuwa unaimbiwa kauli za kukudumaza na kukukatisha tamaa, nguvu ya\\\\r\\\\nndani yako haiwezi kuamka.

Tushukuru sasa mazingira ya kuamsha uwezo\\\\r\\\\nmkubwa ulio ndani ya kila mmoja wetu yamewekwa wazi kwa kila mtu. Alfred\\\\r\\\\nMwanyika kupitia kitabu hiki cha AMSHA UWEZO WAKO HALISI, ametutengenezea\\\\r\\\\nmazingira mazuri ya kila mmoja wetu kuweza kutambua uwezo mkubwa ulio ndani\\\\r\\\\nyetu, kuuamsha na kuutumia kufanya makubwa.

Kitabu hiki ni jawabu la uhakika kwa kila mtu\\\\r\\\\nambaye haridhishwi na maisha anayoishi sasa. Iwe ni kazi au biashara ambayo mtu\\\\r\\\\nanaifanya na haipendi, kipato ambacho hakitoshelezi au mahusiano ambayo yana\\\\r\\\\nmigogoro mingi. Majibu yote ya changamoto hizo tayari yapo ndani yako. Lakini\\\\r\\\\nkwa bahati mbaya sana, hakuna mahali umewahi kufundishwa jinsi ya kupata majibu\\\\r\\\\nyaliyo ndani yako.

Kwenye kitabu hiki, mwandishi ametufundisha\\\\r\\\\nhatua kwa hatua jinsi ya kulitambua kusudi la sisi kuwa hapa duniani, kuweka\\\\r\\\\nmalengo ambayo tunayafanyia kazi na kuweza kuisikiliza sauti ya ndani ambayo\\\\r\\\\ninajua mambo mengi mno kutuhusu sisi.

Tunaweza kukiita kitabu hiki mwongozo wa\\\\r\\\\nmtumiaji (user’s manual) kwenye eneo la uwezo wa binadamu. Iko hivi, ukienda\\\\r\\\\nkununua kifaa chochote kile, iwe ni simu, tv, friji na vinginevyo, huwa unapewa\\\\r\\\\nkijitabu kidogo ambacho kina mwongozo wa jinsi ya kutumia kifaa hicho.

Lakini mtoto mdogo anapozaliwa, haji na\\\\r\\\\nkijitabu chenye maelezo kuhusu uwezo mkubwa ulio ndani yake. Hivyo wazazi, walezi\\\\r\\\\nna jamii kwa ujumla wanashindwa kujua mtoto huyo ana uwezo gani hasa. Wanaweza\\\\r\\\\nkubahatisha kwa kuangalia anapenda vitu gani, lakini hawawezi kujua kwa\\\\r\\\\nuhakika.

Tatizo linakuja pale mtoto anapokwenda shule,\\\\r\\\\nkwani ndipo ule uwezo wake unazikwa kabisa. Maana shuleni anashindanishwa na\\\\r\\\\nkulinganishwa na watoto wengine, ambao hawana uwezo kama alionao yeye. Na hapo\\\\r\\\\nmtoto anapokea kile ambacho anakuwa ameambiwa kulingana na mashindani\\\\r\\\\naliyowekwa. Kama amewashinda wenzake shuleni ataambiwa ana akili na kama wenzake\\\\r\\\\nwamemshinda ataambiwa hana akili.

Kama ambavyo mwanasayansi Albert Einstein\\\\r\\\\namewahi kusema, kila kiumbe ana akili, lakini kama utawashindanisha samaki na\\\\r\\\\nnyani kupanda mti, samaki ataishi maisha yake yote akiamini ni mjinga kwa\\\\r\\\\nsababu ameshindwa na nyani kwenye kupanda juu ya mti.

Hicho ndicho kinachotokea kwenye jamii zetu,\\\\r\\\\nwatu wasioweza kujua uwezo mkubwa ulio ndani ya mtu, wanamweka mtu huyo kwenye\\\\r\\\\nkundi la kushindwa. Kwa sababu ni watu wenye mamlaka juu yake, hasa anapokuwa\\\\r\\\\nmtoto, anakubaliana na hilo na kuyaona hayo ndiyo maisha yake.

Haijalishi umepitia nini, kitabu hiki\\\\r\\\\nkinatufundisha kwamba nguvu ile kubwa bado ipo ndani yetu, imelala tu. Na\\\\r\\\\nwajibu wetu ni kuamsha uwezo huo na kuutumia kuishi maisha ambayo yatakuwa na\\\\r\\\\nmanufaa makubwa kwetu na kwa wengine.

Japo wazazi wako hawakupewa mwongozo wa\\\\r\\\\nmatumizi yako wakati wanakuzaa, wewe umepewa mwongozo huo. Mwongozo huo tayari\\\\r\\\\nupo ndani yako, upo kwenye sauti ambayo imekuwa ndani yako na haitulii. Lakini\\\\r\\\\nkutokana na mahangaiko na usumbufu wa dunia, umejifunza kuipuuza sauti hiyo na\\\\r\\\\nhivyo kushindwa kujijua mwenyewe kwa undani.

Kitabu hiki kinatufundisha umuhimu wa kuwa na\\\\r\\\\nmuda tulivu ili kuweza kuisikiliza sauti ya ndani ambayo ni mwongozo muhimu\\\\r\\\\nkwetu kuweza kufikia uwezo wetu mkubwa.

Kwenye kitabu nilichoandika, kinachoitwa UNA\\\\r\\\\nNGUVU YA KUTENDA MIUJIZA, nimeshirikisha jinsi unavyohitaji utulivu mkubwa ili\\\\r\\\\nkufikia na kutumia nguvu kubwa ambazo tayari zipo ndani yako. Kwenye kitabu\\\\r\\\\nhicho kuna mazoezi mbalimbali kama ya tahajudi, ambayo pia yameelezewa kwenye\\\\r\\\\nkitabu hiki cha AMSHA UWEZO WAKO HALISI.

Kitu kingine muhimu sana unakwenda kujifunza\\\\r\\\\nkwenye kitabu hiki ni kuacha alama hapa duniani. Watu wengi wamekuwa wanapita\\\\r\\\\nhapa duniani kimya kimya. Yaani wanazaliwa, wanaishi maisha ya kawaida na kisha\\\\r\\\\nkufa. Wanasahaulika haraka baada ya kufa kwa sababu wanakuwa hawajatumia uwezo\\\\r\\\\nmkubwa ulio ndani yao kuacha alama yoyote hapa duniani.

Kitabu kimetufundisha njia moja ya uhakika\\\\r\\\\nkabisa ambayo kila mmoja wetu anaweza kuitumia kuacha alama hapa duniani, hivyo\\\\r\\\\nkuendelea kukumbukwa hata baada ya kufa. Huhitaji uwe raisi wa nchi,\\\\r\\\\nmwanamapinduzi au hata tajiri mkubwa ndiyo uweze kuacha alama hapa duniani.\\\\r\\\\nKulijua na kuliishi kusudi la maisha yako ni njia ya uhakika ya kuacha alama\\\\r\\\\nhapa duniani na vizazi vikaendelea kukukumbuka.

Nikupongeze sana kwa hatua uliyochukua ya\\\\r\\\\nkupata kitabu hiki cha AMSHA UWEZO WAKO HALISI, kwa kukisoma kitabu hiki na\\\\r\\\\nkuchukua hatua ambazo mwandishi ameshirikisha, hutabaki vile ulivyo sasa.\\\\r\\\\nMaisha yako yanakwenda kubadilika kwa namna chanya na yatakuwa na mchango\\\\r\\\\nmkubwa kwa wengine.

Kocha Dr. Makirita Amani,

Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio,\\\\r\\\\nMwandishi Na Mjasiriamali.

\\\\r\\\\n\\\\r\\\\n\\\\r\\\\n\\\\r\\\\n\\\\r\\\\n\\\\r\\\\n\\\\r\\\\n\\\\r\\\\n\\\\r\\\\n\\\\r\\\\n\\\\r\\\\n\\\\r\\\\n\\\\r\\\\n\\\\r\\\\n\\\\r\\\\n\\\\r\\\\n\\\\r\\\\n\\\\r\\\\n\\\\r\\\\n\\\\r\\\\n\\\\r\\\\n\\\\r\\\\n\\\\r\\\\n\\\\r\\\\n\\\\r\\\\n\\\\r\\\\n\\\\r\\\\n\\\\r\\\\n\\\\r\\\\n\\\\r\\\\n\\\\r\\\\n\\\\r\\\\n\\\\r\\\\n\\\\r\\\\n\\\\r\\\\n\\\\r\\\\n\\\\r\\\\n\\\\r\\\\n\\\\r\\\\n\\\\r\\\\n\\\\r\\\\n\\\\r\\\\n\\\\r\\\\n\\\\r\\\\n

www.amkamtanzania.com

More Products On Discount
Best Sellers List
Best Seller
10,000 Tsh.
(5.4)

Sold by: Gaston Ngailo

Best Seller
10,000 Tsh.
(69.8)

Sold by: Samuel Macha

Best Seller
3,000 Tsh.
(16.4)

Sold by: ABDULKADIR MASSA

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PETER TARIMO

Best Seller
4,000 Tsh.

Sold by: Mashaka Khamis

GetValue Recommendations
Old is Gold