ALAMA ALIZOACHA HAYATI JOHN POMBE MAGUFULI
Hiki nikitabu kinachoa angazia miaka 5 ya uongozi wa Rais John Pombe Magufuli katika mambo mbalimbali. Nikitabu ambacho kinatakiwa kuwa chachu ya historia ya mambo aliyofanya Rais Magufuli,rnrnNimepata msukumo wakuandika kitabuhiki ikiwa nimsukumo wa ndani kwa jinsi nilivyo vutiwa na mambo aliyo yafanya John Pombe Magufuli. Ni wazi zikiachwa chuki binafsi na masuala ya kisiasa n.k. rnrnRais Magufuli alifanya mambo mengi mazuri ambayo niyakukumbukwa kwa namna yake. Sera zake hata namna alivyokuwa akiongoza nitofauti na awamu nyingine na hakuna Rais ambae amewapa watanzania ujasiri kama Rais John Pombe Magufuli tuki muweka pembeni Baba wa taifa, rnrnNiwazi kuwa Magufuli alikuwa binadamu kama walivyo wanadamu wengine hawezi kukosa mahali ambako alikosea hiyo ni katika ubinadamu kwasababu hakuna ambae amekwisha kamilika kwa asilimia zote hayupo mwanadamu wa namna hiyo duniani. rnrnKatika uhalisia wa mambo Rais Magufuli hakuwa mtu aliyependwa na watu wa tabaka la juu unaposoma kitabu hiki kitakupa nisababu gani zilizopelekea yeye kutopendwa na tabaka hilo ukilinganisha na viongozi wengine waliopita ukiachia mbali Julius Kambarage Nyerere.rn rnNilazima kukubalikuwa pengo la Magufuli ukiachia mbalia la Baba wa Taifa halita zibika kiurahisi hata kama litazibika itachukua miaka mingi kupatikana kiongozi mwenye maamuzi ya aina ile yaliyo shuhudiwa na watanzania. rnrnKuna sababu nyingi zakumuweka Magufuli kwenye maandishi katika milengwa mbalimbali, Niwazi janga la Corona ilikuwa tishio la dunia lakini Magufuli aliweza kuionyesha dunia kuwa Corona si kitu. rnrnMaisha yaliendelea kazi zilifanyika wakati duniani wengine wakiwa katika kufungiwa Tanzania ilikuwa ‘’HAPA KAZI TU’’ Mungu alaze roho ya Rais wetu mpendwa John Pombe Magufuli mahalipema peponi Amina.
Ukweli kuhusu Magufuli ni Rais ambaye ameacha alama kubwa kwa Afrika na atakumbukwa pengo lake huwenda lisizibike kwa wepesi. John Pombe Magufuli hata historia yake na maisha yake mpaka kuwa Rais nikama muujiza wengi hawakutarajia hata yeye hakutarajia. Rais mzuri sikuzote niyule ambaye watu hawakumfikilia wala kumtarajia na viongozi wa namna hiyo ndio waleta mabadiliko katika Taifa fuatilia kitabu hiki.