AKIBA NA UWEKEZAJI
Mwongozo Maalumu kuhusu Akiba na Uwekezaji utakaokufikisha kwenye uhuru wa kifedha.
Akiba na Uwekezaji.
Bilionea na mwekezaji nguli duniani bwana Warren Buffet aliwahi kunukuliwa akisema kwamba \"Usiweke akiba kile kilichobaki baada ya kutumia, lakini tumia kile kilichobaki baada ya kuweka akiba.\"
Kwa maneno hayo ya bilionea huyu ni kana kwamba alikuwa akituambia kuwa ni marufuku kutumia fedha kabla ya kuweka akiba, yaani unapopata tu fedha, jambo la kwanza unalopaswa kufanya ni kuweka akiba na baada ya hapo ndio ufanye mambo mengine kwa fedha iliyobaki.
Bilionea huyu akaendelea kusema kwamba \"Kama hutatafuta njia za kupata fedha hata ukiwa umelala, basi utaifanyia kazi fedha mpaka utakapokufa.\"
Kwa maneno hayo makali, bilionea huyu alitutaka tuelewe kuwa, kama tunataka tusiwe watumwa kwa fedha basi tufanye uwekezaji, hii ni kwa sababu kwenye uwekezaji fedha fedha zinatufanyia sisi kazi.
Kuweka akiba na hata kufanya uwekezaji wala sio jambo rahisi, hivyo basi unatakiwa uwe na maarifa sahihi kuhusu akiba na uwekezaji.
Kwenye kitabu cha AKIBA NA UWEKEZAJI kilichoandikwa na Mwandishi sio Nguli ila mwenye nidhamu kubwa Ndugu Patson chaula Utajifunza hatua kwa hatua jinsi ya kuweka akiba na jinsi ya kufanya uwekezaji kwa usahihi na kuweza kufanikiwa.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza