Mambo 55 Ya Kuzingatia Kabla Ya Kuanzisha Biashara
Ukienda shuleni kuna sheria fulani ambazo lazima uzifuate. Ukitaka kuwa dereva kuna sheria za barabarani ambazo unapaswa kuzizingatia. Ukitaka kuwa rubani lazima ujifunze kuendesha ndege na uzijue kanuni ambazo zinatumiwa na marubani. Sasa suala hili hapa halijaachwa nyuma katika biashara. Ili uweze kuendesha biashara nzuri sana ambayo imesimama na ambayo itaenea katika maeneo mengi hapa duniani basi huna budi kuhakikisha kwamba unajifunza kanuni, mbinu na sheria za biashara. Kwa kulitambua suala hili hapa, basi kurasa za kitabu hiki hapa zimelenga katika kuhakikisha kwamba zinakupatia mambo ya msingi sana ambayo unayahitaji kuhakikisha kwamba unayazingatia kabla ya kuanzisha biashara. Kama ilivyo kweli kwamba mwanafunzi akienda shuleni na asipofuata sheria za shule husika anaweza kupoteza shule hiyo kwa kufukuzwa. Vivyo hivyo kwa mambo ambayo yamo kwenye kurasa za kitabu hiki. Kadri unavyokuwa unazidi kuyakosa ndivyo unavyokuwa unazidi kuididimiza biashara yako. Na kama mambo haya hutayafahamu mapema na kuhakikisha kwamba umeyarekebisha basi sichelei kusema kwamba upo katika njia ya kuipoteza biashara. Wakati shuleni mwanafunzi anafukuzwa na mwalimu kwa ukosefu wa nidhamu au kwa kutotimiza wastani wa maksi zilizohitajika au kwa kufuata baadhi ya sheria za shule husika. Katika biashara wateja ndio walimu.Hawa wanaweza kukufuza aukukuacha. Swali la msingi ambalo unapaswa kujiuliza ni lini wateja watakufukuza. Basi jibu la swali hilo limo katika kurasa za kitabu hiki. Yaani kitabu hiki kina kila kitu ambacho unahitaji kujua kabla ya wewe kuanzisha biashara na baada ya kuanzisha bishara. Kisome kitabu hiki hapa kwa umakini. Lakini pia zitumie mbinu zilizoandikwa kwenye kurasa za kitabu hiki hapa kuhakikisha kwamba unaanzisha, unakuza na kuisambaza biashara yako popote pale unapotaka. Asante sana, Tukutane kwenye meza ya wanamfanikio Godius Rweyongeza
Karibu sasa ujipatie nakala yako
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza