Your Basket

Checkout | Shopping Cart
uelewa wetu wa maarifa unapoua uelewa wetu wa mwili || GetValue

UELEWA WETU WA MAARIFA UNAPOUA UELEWA WETU WA MWILI

UELEWA WETU WA MAARIFA UNAPOUA UELEWA WETU WA MWILI

Siku hizi maisha yetu yametawaliwa na sheria na kanuni tunazopata kutoka kwenye maendeleo yetu ya maarifa kwa jinsi tunavyo fikiri na kutafuta ubora wa maisha tunavyo ishi. Vitu vingi tumevichambua kwa faida na hasara kutokana na mahitaji yetu tunavyo hisi tunahitaji kuwa bora. Kila siku tunaongeza maarifa kufikia kupata masuluhisho na majibu ya tamaa zetu kwa tunavyo hisi ni sahihi.

Tumeona uelewa wetu wa maarifa upo kukidhi tunachotaka kutimiza kwa matakwa yetu kimawazo na hisia kwajinsi tunavyoishi. Je, tunavyoishi ni sawa na miili yetu inatakiwa kuwa kwa kuitimizia mahitaji yake. Tuna uhakika na tunachokitimiza kinatatua tatizo letu au ni tatizo zaidi ndani ya miili yetu. Tukijipa furaha ya kuilisha hisia kimawazo kwa mafanikio hayo yanaendana na miili yetu inavyo takiwa kutendewa.

Ina maana gani tukisema uelewa wa mwili tumeshaona uelewa wa maarifa jinsi unavyofanya kazi. Mwili una uelewa wake ambao ndio nguzo ya utendaji kazi wake. Na uelewa huo huwa nnje ya kufahamu kwetu na maamuzi yetu tuyoweza kufanya kwa kufikiria. Kwa ujumla mwili wetu unavyo tenda kazi hakuna anayeweza kufahamu wala kuamua ndani yake. Na hii ni siri kubwa ya ulimwengu inayotufanya kutuweka salama zaidi kuliko tungeweza kuwa na maamuzi juu ya miili yetu ndani itendaje.

Uelewa wa miili yetu unaweza kudhurika kutoka na mwenendo wetu mbaya kwa jinsi tunavyo utendea mwili. Tunatumia uelewa wa maarifa yetu kuudhuru mwili wetu kwa matakwa yetu binafsi yasiyokuwa na tija kwenye afya zetu. Ubora wa uelewa wetu wa mwili hushuka pale tunapo ulazimisha mwili kwenda tofauti na asili yake inavyotaka. Kuna mengi tunayotenda kwa jina la kujituliza na kujikamilisha na yanakuwa na matokea mabaya sana kwenye kuua uelewa wetu wa mwili unaohitajika kutuweka sawa afya yetu ya mwili.

Kwa mfano tuna mawazo tofauti ya jinsi tunavyotakiwa kufurahia mapenzi kwa kila siku tunatengeneza na kutumia vitu vitavyorefusha muda zaidi kwakuhisi ndio furaha tunaifikia lakini ukweli ni tunaenda kinyume na asili yetu ilivyo na kuharibu uelewa wa miili yetu kwa kuilazimisha isivyopaswa kwa ujinga na tamaa yetu. Kukosa muda sahihi wa kulala kupumzisha mwili huchangia kuharibu ufanisi wetu na jinsi ulaji wetu ulivyo tunakula na kunywa vitu visivyo na faida kwetu. Hata mvurugano kutokuwa na akili iliyotulivu na kuchanganyikiwa na mawazo na hisia kwa muda mrefu ni tatizo pia kweye afya ya miili yetu.

Tunahitajika kuwa makini sana kwakuwa hakuna tunachoweza kufanya wala kuwa na maarifa zaidi ya uelewa wa miili yetu yenyewe kwenye kutimiza majukumu yake ya kuulinda mwili. Kutofanya mambo yatayo punguza uwezo wake si hiari kwetu kama tunataka afya bora na maisha yasiyo na udhaifu mkubwa wa mwili. Hakuna mbadala wa uelewa wa miili yetu ni kazi ya ulimwengu yenyewe na uwezo wake na maarifa yetu hatogusa eneo hilo kabisa. Hatuna bidi kuchukua muda wetu kujitathmini tunapenda uzima wa miili yetu au kutimiza furaha ya mawazo yetu tu.

Nb: Kila siku uelewa wetu wa maarifa unapanda sana na uelewa wa miili yetu ndio tunavyozidi kuuharibu. Hatujajua tunafaidika au tunapata hasara kubwa upande mwingine. Hatujui usawa uko wapi wakwenda na vyote sambamba. Tuone tutafikia wapi na tunapata matokeo gani mbele ya safari. 


Fungua link kujifunza zaidi,

https://lastphilos.wixsite.com/psyche/post/uelewa-wetu-wa-maarifa-unapoua-uelewa-wetu-wa-mwili

Ratings: (0) Leave a Comment

You must login to post your comment.

Post Posting...