NDOTO YAKO INAWEZEKANA
Kitabu hiki ni mahususi kwa kila mtu ambaye ana ndoto ya kuwa mtu fulani au kufanya kitu fulani. Utakapo soma kitabu hiki na kufanyia kazi mafunzo yaliyopo ndani yake, ndoto yako itakuja kwako kwa wepesi usiodhani. Kwa kifupi, kitabu hiki ni mafunzo ya namna ya kutambua na kutimiza ndoto yako; kimeandikwa kwa namna ya kipekee ambayo sio nadharia lakini ni mpango mkakati uliotokana na mwandishi kutimiza ndoto zake na wengine alio wafundisha kutimiza ndoto zao.
Kutimiza ndoto ni kama safari ya kwenda mahali; kutoka ulipo sasa mpaka mahali ndoto yako inatimia ni SAFARI.
Utahitaji CHOMBO cha usafiri, utahitaji kulipa GHARAMA, utahitaji kujua MWELEKEO na kufahamu kuwa itachukua MUDA ili kufika pale ndoto yako itakapotimia.
Ni vyema kufahamu kuwa, kwenye safari ya kutimiza ndoto, tusing’ang’anie tu kule tunako kwenda tu (HATIMA| MWISHO), tukumbuke kuwa hata NJIA (na mambo yanayo fanyika njiani) ni sehemu muhimu ya kutimiza ndoto yako.
Kuna mambo muhimu hutokea unapokuwa njiani ambayo yana sehemu kubwa katika kukuandaa KITABIA na MWENENDO ili uweze kuhimili MAISHA utakayoishi ukisha itimiza ndoto yako.
Ndio maana ni muhimu ukajipanga, ukachagua njia utakayotumia, chombo utakachotumia na pia angalia gharama ulizo tayari kulipa; usije ukafika kwenye ndoto yako ukakuta umelipa gharama kubwa kuliko unavyoweza kustahimili.
Kitabu hiki kitakusaidia HATUA kwa HATUA, sura kwa sura namna gani utaweza kujitambua, kutambua ndoto yako, kuiamini na kuitimiza.