Your Basket

Checkout | Shopping Cart
jinsi ya kuongeza thamani yako || GetValue

JINSI YA KUONGEZA THAMANI YAKO

JINSI YA KUONGEZA THAMANI YAKO

Rafiki yangu mpendwa

Salaam,

Moja ya kitu muhimu sana unachopaswa kukifanyia kazi kwenyernmaisha yako ni thamani yako. Ila kwanza labda tujiulize thamani ni nini? Ilirntujue maana halisi ya thamani nimelazimika kuangalia kwenye kamusi ya Kiswahilirnsanifu, ambayo inasema Kuwa thamani nirngharama au ubora wa kitu kutokana na hali na kuhitajika kwake na jamii.

Sawa hiyo ni maana ya thamani, na je, ipi itakuwa maana yarnthamani binafsi. Thamani yako tunaweza kuiona kwa kuangalia vitu viwili muda na kiasi cha pesa unacholipwa ndani ya huo muda. Kwa mfano, kuna mturnkwa siku anaingiza kipato cha milioni kumi. Wakati kuna ambaye anaingiza kipatorncha laki moja. Na wakati huohuo kuna ambaye hata elfu kumi hapati.

Kumbe hawa watu watatu thamanirnyao binafsi haiwezi kuwa moja. Pengine unajiuliza, imekuwaje mimi nimeamuarnthamani ya mtu ipimwe kwa kiwango cha fedha anachoingiza. Ukweli ni kuwa siyornmimi niliyegundua hili. Hiki ni kitu ambacho watu wengi wamekuwa wanakitumiarnkutoa thamani kwa watu, na hata kwenye familia nyingi mtu mwenye pesarnanathaminiwa sana kuliko ambaye hana fedha.

Vikiitishwa vikao vya familia, kama kuna kuna watu wawili,rnmmoja mlevi mlevi na mwingine ni mtu ambaye anafanya biashara na ana kipatornkizuri. Ikitokea mlevi akachangia kitu, watu watasema huo ni ulevi hata kamarnkaongea pointi ya maana, ila mwenye hela hata akiongea pumba, anaonekanarnameongea pointi na hata kupigiwa makofi. Chezea hela wewe! Mtu mwenye hela yakernanaitwa bosi mkubwa hata kama nirnmdogo. Hahaha.

Sasa kwa kwa vile tunaishi kwenye dunia ambayo inathamanisharnwatu hivyo, hatuna budi kujua hili ili tuongeze thamani zetu au wewe unasemaje?rnWewe pia unapaswa kujua thamani yako kwa sasa hivi, lakini pia unapaswa kufanyarnjuhudi ili kufanya thamani yako iongezeke zaidi.

Mbinu unazoenda kujifunza kwenye kitabu hiki zitakusaidiarnkuongeza thamani yako mara mbili mpaka mara kumi zaidi. Yaani, utaweza kulipwarnmara mbili mpaka mara kumi zaidi ya unavyolipwa sasa hivi. Kumbe basi naombarnnieleweke kwenye suala moja tu, ninaposema kwamba unaenda kujifunza mbinu zarnkukusaidia wewe kuongeza thamani yako. Simaanishi kwamba, utaongeza thamani kwarnkuwa mrembo zaidi. Wala simaanishi kwamba utaongeza thamani kwa kupata followers zaidi mtandaoni, na walarnsimaanishi kwamba unaongeza thamani yako kwa kuwa mrefu, mfupi, mtu wa mirabarnminne, mweusi, mweupe au maji ya kunde!

Bali namaanisha kuongeza thamani kwa kulipwa zaidi. Ukitumiarnmbinu zilizoainishwa kwenye hiki kitabu, utakuwa na uwezo wa kulipwa mara mbilirnmpaka mara kumi zaidi. Hivi kwa mfano unaanzaje kuacha kutumia mbinu hizi ilirnuweze kulipwa zaidi ya unavyolipwa sasa hivi.

Kabla hatujazama zaidi kwenye kitabu, ngoja kwanza tuonernnamna unavyoweza kujua thamani ya muda wako kwa sasa

Jinsi Ya KujuarnThamani Ya Muda Wako

Mimi na wewe tuna bahati ya kuwa na rasilimali nyingi ambazorntunaweza kutumia kwenye maisha yetu ya kila siku.

Rasilimali hizo ni kama

<!--[if !supportLists]-->·       rn<!--[endif]-->Ardhi

<!--[if !supportLists]-->·       rn<!--[endif]-->Madini

<!--[if !supportLists]-->·       rn<!--[endif]-->Maji

<!--[if !supportLists]-->·       rn<!--[endif]-->Fedha

<!--[if !supportLists]-->·       rn<!--[endif]-->Muda ……

Kati ya hizo rasilimali zote, muda ndio rasilimali ambayo ukiipotezarnhuwezi kuipata. Hivyo, unahitaji kuweza kuitumia vizuri rasilimali hii yarnkipekee.

Na leo nataka nikwambie namna ambavyo unaweza kujua thamanirnya muda wako. Kujua thamani kutakusaidia zaidi kuwekeza nguvu zako kwenyernkufanya kazi na majukumu ambayo ni ya muhimu, huku ukiachana na majukumu ambayornsiyo ya muhimu

Ili tujue thamani ya muda wako, kwanza unapaswa kujua kiasirngani unataka kuingiza kwa mwaka mmoja ujao. Ebu kwa mfano tuseme kwamba unarnmpango wa kuingiza milionoi 100. (Hiki kitu tukiite A)

Kitu cha pili cha kujiuliza ni muda kiasi gani ambao ukorntayari kufanya kazi kwa wiki? Kama kwa siku unafanya kazi kwa saa 15 na kwarnwiki unafanya kazi kwa siku sita. Maana yake kwa wiki unafanya kazi kwa saa 90rn(Hiki kitu tukiite B).

Na kitu cha tatu ambacho tunataka tujue ni je, kwa mwakarnutakuwa tayari kufanya kazi kwa wiki ngapi? Kwa kawaida mwaka una wiki 52. Sasarnni wiki ngapi utakuwa tayari kufanya kazi ukiondoa wiki za mapumziko. Kamarnunapumzika kwa mwezi mzima kwa mwaka, maana yake unafanya kazi kwa wiki 48 turnkwa mwaka (hiki kitu tukiite C).

Sasa kifuatacho, ngoja tuone thamani ya muda wako kwarnkutumia vipengele hivyo hapo juu. Kujua thamani ya muda wako utachukua.

Thamani ya saa lako moja= (A÷B÷C)

Kwa hiyo kama una mpango wa kuingiza milioni 100 (100,000,000)rnkwa mwaka na upo tayari kufanya kazi kwa saa 90 kwa wiki kwa wiki 48. Hivyo,

Thamani ya saa lako moja=(100,000,000÷90÷48)=23,146

Kwa hiyo wewe thamani ya saa moja kwako ni sawa na 23,148.rnUkifanya kazi yoyote ambayo ni ya chini ya hivyo viwango, basi unakuwarnumejishusha.

Kama ulikuwa hujawahi kupima thamani ya muda wako, Ebu fanyarnhivyo siku ya leo. Utajifunza vitu vingi na kikubwa zaidi ni kwenye utunzajirnmzuri wa muda wako ili kazi unazofanyaa ziendane na viwango vya thamani yako.

Lakini ubora ni kwamba unaweza kuongeza thamani ya saa lakornmoja kutoka kiwango cha chini na kukipandisha juu kabisa.

Hakuna kiwango cha ukomo wa thamani ya muda wako unachowezarnkutengeneza

Sasa wacha tuzame ndani zaidi kwenye hiki kitabu ili uwezernkuona ni kwa namna gani unaweza kuongeza thamani yako hatua kwa hatua. Mbinurnunazoenda kujifunza kwenye hiki kitabu ni mbinu ambazo wanatumia waturnwanaolipwa kiwango kikubwa cha fedha kwa siku, wiki na mwezi. Ubora ni kuwarnmbinu hizi ukizitumia wewe mwenyewe unaenda kupata matokeo makubwa ambayo hatarnhapo awali ulikuwa hujafikiria kuwa unaweza kuyapata.

Miaka kadhaa iliyopita nilikuwa namsikiliza Les Brown,rnkwenye yale maongezi akawa anasema kwamba alipokuwa anaitwa kwenye seminarnalikuwa analipwa dola elfu moja kwa kila maongezi. Ila sasa siku moja katikarnkuongea na baadhi ya watu waliokuwa wanatengeneza kiasi kikubwa zaidi ya hapo,rnwalimwambia kuwa unaweza kulipwa zaidi ya hapo. Wakamwambia kuwa badala yarnkulipwa dola elfu moja unaweza kulipwa mpaka dola elfu tano kwa saa moja. LesrnBrwon anasema kwamba hiki kitu kilimpa hofu kwanza, lakini baadaye alipoanzarnkukifanyia kazi, kitu hiki kikaleta matokeo makubwa akawa ameanza kulipwa hichornkiasi na baadaye akaweza kulipwa zaidi ya hapo.

Ninachotaka kukwambia ni kuwa, unaweza kulipwa zaidi yarnunavyolipwa sasa hivi. na mbinu zilizoainishwa kwenye hiki kitabu zinajielezarnwaziwazi tu.

Wasalaam,

Ku

Kupata kitabu BONYEZA HAPA


https://www.getvalue.co/prod/jinsi_ya_kuongeza_thamani_yako
Godius Rweyongeza

0755848391

Morogoro-Tz

24 Agosti, 2022.


uNAWEZA KUJIFUNZA ZAIDI KUTOKA KWANGU KUPITIA

https://www.songambele.co.tz/


AU BONYEZA HAPA


rnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrn

 

Ratings: (0) Leave a Comment

You must login to post your comment.

Post Posting...