JE UNAUPOTEZA MUDA WAKO AU UNAUWEKEZA?
Mtu mmoja akanipigia Simu na kuniambia, "kaka Tungaraza, Ahsante sana kwa masomo yako ya Mtandaoni, yamenisaidia kwa sehemu. Ila Nina shida moja, naona kama napoteza tu muda hapa Duniani. Nisaidie."
Nikawaza, "huyu ni nani tena muda huu wa Asubuhi!"
Nikaamua nimuulize Swali...
"UNAPOTEZAJE MUDA?"
"Kila ninachokifanya, naona hakina manufaa," akanijibu, "na wala havinipi pesa."
"Aaah, Kumbe hiyo ndiyo shida?" Nikaamua kumuuliza tena.
"Ndiyo, hiyo ndiyo shida inayonitesa sana."
"Okay, sasa naomba unisikilize, nikusaidie kwa sehemu." Nikaendelea.
"Siyo kila unachokifanya na kikashindwa kukupatia Pesa, huwa ni kupoteza Muda. Hapana."
"Kupoteza muda (Wasting time) ni kufanya au kushiriki kwenye Jambo lisiloendana na Kusudi la Mungu katika maisha yako; Yaani, kusudi la kuzaliwa kwako. Au Jambo lisiloendana na Maono yako, au Ndoto zako za kimaisha, au mipango na Malengo yako."
"Ikiwa unafanya au unashiriki kwenye Jambo linaloendana na niliyoyataja hapo juu, basi hupotezi Muda wako, Bali unauwekeza muda wako (you are Investing your time)"
"Umeelewa?"
"Ndiyo, ila Kidogo. Sasa nifanye hadi lini kama sipati pesa?" Akaniuliza tena.
"Ok. Fanya mpaka pale utakapopata unachokitafuta."
"Lakini Inawezekana pia hupati Matokeo chanya kwa Sababu unafanya kitu sahihi kwa kutumia Njia zisizosahihi. Hivyo, chunguza njia unazotumia kama ni sahihi. Pamoja na kiwango cha jitihada unachotumia katika kufanya kazi yako."
"Hapo nimekupata, Ahsante sana kaka yang, Mungu akubark. Nitakujulisha." Akajibu na kuhitimisha mazungumzo yetu.
Hivyo ndivyo ilivyokuwa.
Sasa...
Je, WEWE NDUGU YANGU...
MUDA WAKO HUWA UNAUPOTEZA au UNAUWEKEZA?
Angalia niliyoyaandika hapo juu ili uweze kujua uko upande gani.
Kwa Ushauri zaidi au kwa mazungumzo ya kunialika mahali, Njoo WhatsApp kwa 0764793105.
BY LACKSON TUNGARAZA.
@lacksontungaraza.
Author | Independent Consultant | High-Income Copywriter.
P.S. Kesho Bora Inatengenezwa Leo. USIUPOTEZE MUDA WAKO.
.