HUWA HUKUNA MVURUGANO KWENYE KUWA MAKINI BALI UTAFSIRI WAKE
Siku hizi kila mtu anatafuta njia tofauti tofauti na wengi wanafundisha unawezaje kuwa makini. Ina onekana kuna tatizo kubwa la watu kushindwa kuwa makini kwenye wanachofanya na kupata mvurugiko kwenye akili zao. Tunashindwa kuwa na akili iliyotulia kwakuwa muda wote tupo kwenye mkanganyiko wa mapigano ndani ya akili zetu wenyewe bila chanzo chochote kutoka nnje.
Embu tujiulize ni kweli kuna vizuizi vinavyoleta mvurugano na kushindwa kuwa makini akilini mwetu. Au kuna kitu kingine tofauti tusichojua kinachotufanya tuone tatizo tunalo litengeneza wenyewe kwa tafsiri zetu. Kutokuwa makini ina maana gani kwetu, akili kushindwa kufuata unachohisi unataka na kuona unalazimika kujilazimisha kutaka unacho pingana nacho, na kwanini hilo litafsirike tatizo la kuwa makini.
Kuna muda unajiona huwezi kuwa makini lakini ghafla ukapata kitu kinachokusisimua ukajikuta umekuwa makini bila kutegemea, hii ina onyesha kuwa makini si jambo la kulazimisha kwa ufahamu wako bali inatokana na ubora na utulivu wa uelewa wa akili yako. Tumekuwa na mabadiliko mengi ya kihisia na mawazo ya ghafla bila kuwa na ufahamu nayo na hatuliwekei uzito swala hilo kulijua kwa undani.
Kwanza tujiulize umakini ni upi? Ni kuweza kutenda kila kitu kwakutaka kwa kulazimisha tuwepo kwenye wakati wa tukio huku ukitumia nguvu ya kufahamu. Umakini haupo kwenye katakwa yetu na hatujui hilo kwa kulamisha kuwepo kwenye wakati ndio hua kizuizi kinacholeta mvurugiko tunao uona ni kutokuwa makini.
Muda wote akili yetu ipo kwenye mwenendo wa mawazo na hisia bila hiari wala matakwa yetu na pakiwa na chakutuweka makini huwa moja kwa moja tunakuwa makini ila kutoelewa kwetu ndio huleta mvurugano kwa kutaka kudhibiti wakati wa tukio na kuleta shida ya kutokuwa makini.
Kwenye uhalisia hakuna mvurugano unao sababisha kushindwa kuwa makini ila ni tafsiri zetu za kuona mwenendo wa mawazo umenda pengine na sisi tukafikiri ni tatizo na kuanza kupingana nalo hapo ndio tunatengeneza kutokuwa makini. Ila ukiweza kuangalia mwenendo wa mawazo na hisia bila kutafsiri kwa kutaka kudhibiti kuwa ni tatizo utaona hakuna tatizo lolote kwenye mwenendo wa umakini wako na akili itabaki tulivu muda wote.
Nb: Tufufue ufahamu wetu na tuanze kuona uhalisia wa mambo ndani ya akili yetu jinsi tunavyo ya tafsiri tofauti na kutudhuru. Utulivu na umakini wetu ni wa muhimu sana katika akili yetu kuweza kutosababisha mivirugano na upotofu wa kushindwa kuona uhalisia wa maisha.