Your Basket

Checkout | Shopping Cart
afya ya akili ni matokeo ya kujitambua undani wako halisi || GetValue

AFYA YA AKILI NI MATOKEO YA KUJITAMBUA UNDANI WAKO HALISI

AFYA YA AKILI NI MATOKEO YA KUJITAMBUA UNDANI WAKO HALISI

Afya ya akili ni neno ambalo tunalisikia sana siku hizi, kila mtu anaweza kuwa na wazo lake kuhusu hili neno. Tukisema afya ina maana ni kuwa sawa katika asili yake. Na akili ni utendaji kazi katika ubongo. Afya ya akili ni akili inapokuwa sawa katika utendaji kazi wa ubongo kwenye mfumo wake bila kujiletea madhara kwake na kwa wengine katika mazingira yake.


Kitu gani kitakuonyesha kuwa hauko sawa kiakili. Je, unaweza mwenyewe ukajitambua au mpka mtu akushtue kuhusu hilo.


Kuna matokeo yana kuonyesha dhahiri kuwa akili yako haiko sawa, kwa jinsi utendaji wake ulivyo katika mkanganyiko tofauti na unavyotakiwa iwe. Matendo yako yakiwa ni ya hofu na wasiwasi, msongo wa mawazo, kushindwa kuelewa hisia zako na kuwa mwathirika nazo, kushindwa kuwa na akili ambayo haipo kwenye kifungo au kizuizi chochote cha mategemeo, kutaka kuwa ama kuwa chini ya mfumo fulani ili kutenda.


Kuishi kwa kuhangaikia vitu vya nnjee yako visivyokuwa na mahusiano ya moja kwa moja na wewe na kukupumbaza kushindwa kujifahamu mwenyewe undani wako inaweza kukupelekea ukawa unaishi kwakutumia nguvu sana na kujichosha akili yako kwakuwa umejiweka kwenye kifungo unachotumikia bila furaha kwenye utendaji wako kwakuwa unatenda tofauti na wewe jinsi ulivyo.


Kutumia nguvu kubwa kuamua na kuchagua katika kufikiri unapotaka ufanye jambo ina maana hujaelewa unachotaka na akili yako haina ubayana. Na hii nikutokana na unataka uwe upande chanya tu na hili tatizo litaloleta kujutia na kubebesha mizigo akili itayoinyima wepesi katika utendaji wake.


Na haimanishi ukiwa unafaulu mitihani na umefanikiwa kifedha ni ishara ya kuwa sawa kiakili hapana, uzima wa akili ni jambo pana na landani yako zaidi ya maarifa uliyonayo. Usi puuzie na kufikiri kuokota makopo, kutembea bila nguo ndio kutokuwa sawa hapana bali kiini cha kutokuwa sawa kwa akili kunaletwa na kushindwa kufahamu muundo wako wa utendaji wako wa ubongo na kushindwa kuwa huru katika kutambua uhalisia na mawazo yako yanayotaka usalama kwenye muda. Na hili kukupelekea kuishi kwenye giza la kutokuwa na ufahamu wa kweli yako ni ipi yenye thamani ya maisha yako.


Ukishajua mwenendo wako wa kiakili na thamani yako kutokea ndani yako mwenyewe na kuiishi nnjee basi umefanikiwa, bila kutambua hilo mwenyewe utapigania kila kitu cha nnje kikupe thamani na utaishi kwa kumiliki vingi na kudhibiti vingi lakini bado hutoweza kupata ladha ya maisha yenye furaha halisi. 


Kuishi uzima wako wote kwenye siku yako kwenye utendaji wako ndio msingi wa maisha wenye kufanya akili yako itumike na ufanisi wake wote bila kufanya kwa mategemeo ya kupata furaha mwisho wa siku. Afya ya akili ni furaha yako yote, uwezo wako wote na thamani yako yote viwe hai kwenye nyakati zote za maisha yako.


Nb: Hakuna mtu anayeweza kukutibu afya ya akili yako, unaweza kupata mbinu na dawa lakini havitoweza kutoa chanzo cha tatizo lako. Ni lazima wewe mwenyewe uweze kuangalia kwa makini mwenendo wako wote wakimawazo na kuuelewa kuwa na ufahamu nao na hapo ndio afya ya akili inapo chanua na kustawi.



Ratings: (0) Leave a Comment

You must login to post your comment.

Post Posting...