Your Basket

Checkout | Shopping Cart
5ni ipi maana ya dini yenye kutukomboa na kutuweka pamoja || GetValue

5NI IPI MAANA YA DINI YENYE KUTUKOMBOA NA KUTUWEKA PAMOJA

5NI IPI MAANA YA DINI YENYE KUTUKOMBOA NA KUTUWEKA PAMOJA

Wakati wetu huu tumekuwa na dini nyingi zenye mifumu tofauti na kupingana zenyewe. Kwa ufupi kwa kuonyesha hili ina maan zina ubinafi ndani yake na hazi husiani na lengo lenye maana halisi ya dini ya kutuweka pamoja na kutuweka huru kwenye maisha.


Kwa mtazamo wenye mantiki, dini ni mfumo ulianzishwa kumtoa mtu kwenye ujinga na kumpa mwangaza wa kujitambua na kuacha kuishi kwenye njozi zinatompotosha na kuanza kuiona dunia kwenye uhalisia wake na kujitambua na yeye ni mthamani wa dunia hii.


Kuamini tu kwa muda wowote ule hakutoenda kukufanya ujitambua na kumaliza ujinga wako wa kutojifahamu. Bali una hitajika uwajibike asilimia zote wewe mwenyewe ili uweze kupata ukombozi wako. Huwezi kumaliza mizizi ya tamaa, ubinafsi, woga, mkanganyiko wa kimawazo katika akili yako kwa kumuamini Mungu tu akufanyie hayo na wewe uamini tu.


Kitu kinachofanya tunakuwa tofauti ni kipi kama Mungu ni mmoja. Kila dini ina kuwa na sheria na njia zake za kufika kwenye ukombozi wa nafsi na kwanini ziwe utofauti wake wakukinzana. Kutokana na kutoelewa kwetu na ubinafsi ndio umetufanya tumejitenga na kutoelewa lengo kubwa la dini kwetu ni lipi. Tunaishia kuwa na uoga wakutojitambua na kuzidi kutuhofisha na kuangukia kuamini kwa kuogopa au kufuata wengine tu.


Nia ya dini ni kukuonyesha wewe ni kitu kimoja na ulimwengu, unathamani kama watu wengine wote, ujitambue uhalisia wako na uishi bila hofu na udanganyifu wakimawazo na unaoupata kutoka katika mazingira yako kwa watu wenye ubinafsi wa kukudhibiti kwa manufaa yao.


Dini haipaswi kukufanya ukawa mtumwa wake kuitumikia ama kujitambulisha nayo na wala kukuweka kwenye ulinganifu wakupingana na wengine. Binadamu hayuko chini ya dini yoyote ile, na wote tuko sawa kwenye asili moja, ujinga wetu unatutenganisha na kutufanya dini ibadilike maana nakuendana na upotofu wetu na kuzidi kututenganisha na kutuweka kwenye utegemezi wake na kuondoa uwajibikaji wakujifahamu zaidi wenyewe.


Tunatakiwa tuwe makini tuweze kuona uhalisia na dini itakuwa msaada kwetu kutuweka huru na kutunganisha pamoja na kutupa nguvu yakukabiliana na mazingira yetu vyema. Ukielewa utaingia kwenye mshangao kwakuwa vitu vyote vyakushawishika ulivyokuwa hujavijua utabaini ni akili yako yenyewe ndio iliyokuwa inatengeneza pingamizi kwakutojitambua utendaji kazi wa mwili wako, jinsi hisia zako na matakwa yake kwenye kuulisha nafsi yako iliyojitengeneza kimawazo.


Usipoweza kujitambua wewe mwenyewe ndani yako na kumuona Mungu ki maana zaidi ya maneno usitegeme mtu atakuonyesha hilo, utaishia kuwa na maneno tu na kutafuta usichokijua kwa kujinufaisha mwenyewe tu.


Tujiulize kwa makini kwanini hakuna anaye omba ili ajitambue awe huru kujielewa uzima wake na tuna ishia kulilia vitu tu na kutegemea mabadiliko ndani yetu . 


Nb: Baraka haziji kwenye kuomba sana kwa kutoa sadaka kubwa bali ni kuweza kuwa na moyo safi wenye masikio na macho yakuona maono unayo pata, yaweza kuwa kiutendaji na ukafanya kitu kitacho mgusa kila mtu na kumsaidia.



Ratings: (0) Leave a Comment

You must login to post your comment.

Post Posting...